Kansela wa Ujerumani azipongeza jumuiya za wafanyakazi
30 Aprili 2023Matangazo
Scholz amewasilisha pongezi hizo baada ya miezi kadhaa ya harakati zilizosababisha vurumai katika uchumi wa nchi. Kansela wa Ujerumani amesema huu ni wasaa wa kusisitiza kwamba maslahi ya wafanyakazi yanapaswa kuwamo katika moyo wa demokrasia.
Amezipongeza jumuiya za wafanyakazi kwa kuyazingatia maslahi ya kijamii na haki za wafanyakazi. Harakati za hivi karibuni za jumuiya hizo zilizoendeshwa kote nchini Ujerumani, ziliathiri huduma za afya, usafirishaji, posta na huduma kadhaa katika sekta nyingine za uchumi.
Soma pia: Kansela Scholz atoa ujumbe wa heshima kwa vyama vya wafanyakazi
Jumuiya hizo zinapigania malipo zaidi kwa wafanyakazi pamoja na mazingira mazuri ya kazini.