Scholz aahidi asilimia 2% ya pato jumla kutumika kijeshi
10 Novemba 2023Matangazo
Scholz aliahidi kwamba asilimia mbili ya mapato jumla ya nchi, daima itaelekezwa kwenye ulinzi katika kipindi kilichosalia cha miaka ya 2020 na baadaye miaka ya 2030.
Asilimia 2 ya pato jumla ya nchi ni kiwango ambacho kimewekwa na jumuiya ya kijeshi ya NATO kwa kila nchi mwanachama. Ili Ujerumani kufikia kiwango hicho, italazimika kutumia zaidi ya euro bilioni 20 kwa ulinzi kila mwaka.
Scholz: Ujerumani kuwekeza zaidi katika sekta ya ulinzi
Wakati wa mkutano na wanajeshi uliofanyika leo, Scholz amesema hazina maalum ya euro bilioni 100 ya Jeshi la Ujerumani ni hatua ya kwanza muhimu.
Alikuwa akizungumzia hazina maalum ya serikali iliyoanzishwa kwa ajili ya kuboresha jeshi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.