1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ziarani nchini Angola

7 Februari 2020

Kansela Angela Merkel anatarajiwa kukutana na Rais wa Angola Joao Manuel Goncalves ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu Kusini mwa bara la Afrika. Ziara ya Merkel inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara.

https://p.dw.com/p/3XPJQ
João Lourenço, Angola Präsident
Rais wa Angola Joao LuorencoPicha: Getty Images/M. Spatari

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Angola Joao Manuel Goncalves huku mazungumzo hayo yakijikita zaidi katika uimarishaji wa uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili lakini muhimu zaidi jukumu la Angola kama mshirika wa kiuchumi katika kanda hiyo.

Merkel ambaye ameongozana na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Ujerumani pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kibiashara kati ya Ujerumani na Angola na baadae kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Kansela huyo wa Ujerumani ambaye ni mkuu wa kwanza wa serikali ya Ujerumani kufanya ziara nchini Angola mnamo Julai mwaka 2011 pia anatarajiwa kuonyesha kuunga mkono mageuzi katika serikali ya Lourenco hususan vita dhidi ya jinamizi la ufisadi.

Nchi hiyo iliyoko Kusini mwa Afrika ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani licha ya kuzalisha mafuta imezongwa na ufisadi.

Wa hivi karibuni kuhusishwa na kashfa za ufisadi ni mwanawe wa kike Rais wa zamani aliyeongoza nchi hiyo kwa muda mrefu Jose Eduardo dos Santos ambaye ametajwa kuwa mwanamke mwenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika.

Isabel dos Santos, amekuwa akichunguzwa kwa tuhuma za kufuja mamilioni ya pesa za umma kutoka kwa kampuni ya mafuta ya serikali ya Sonangol alipokuwa mwenyekiti.

Merkel alifanya ziara Afrika Kusini na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa

Besuch von Bundeskanzlerin Merkel in Südafrika
Kangela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Alhamisi, Merkel alifanya ziara Afrika Kusini ambapo alifanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa kuhusu namna ya kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

"Ninafahamu kuwa munafanya kila kitu ili kuvutia wawekezaji. Najua kuwa wajumbe hawa wanapanga kuwekeza hapa. Hata hivyo, inabidi kufanyike mazungumzo ili kuondoa vikwazo kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika na fursa hizi za uwekezaji,"amesema Merkel.

Katika ziara yake Afrika Kusini, Merkel aliyatolea wito mataifa ya Afrika kuwa katika mstari wa mbele kutafuta suluhu ya mizozo nchini Libya. Nchi hiyo imekuwa katika msukosuko tangu kupinduliwa kwa kiongozi wake kanali Moamer Gaddafi mnamo mwaka 2011. Ujerumani iliandaa mkutano mjini Berlin uliolenga kuyapatanisha makundi yanayohasimiana nchini humo.

Aidha, Merkel pia alifanya mkutano na wafanyabiasha kutoka Ujerumani na Afrika kusini na pia kukutana na wanafunzi wa chuo kikuu cha Pretoria.

 

Vyanzo/DPA/