1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani aitembelea Romania

3 Aprili 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameitembelea Romania hii leo kwa lengo la kuonesha uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa mshirika wake huyo muhimu wa jumuiya ya NATO anayepakana na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4PeJe
Rumänien Bukarest | Olaf Scholz und Klaus Iohannis
Picha: Andreea Alexandru/AP Photo/picture alliance

Ziara hiyo pia ni ya kuonesha mshikamano na Moldova ambayo ni jirani wa Romania na ambayo inaonekana hasa kuwa katika nafasi hatari  tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka jana.

Rais wa Moldova Maia Sandu ambaye anaituhumu Moscow kwa kuchochea machafuko katika nchi yake anatarajiwa pia kujiunga na kansela Scholz pamoja na rais wa Romania Klaus Lahannis katika  mkutano utakaofanyika baadae mjini Bucharest.

Mazungumzo ya viongozi hao yanatarajiwa kujikita kwenye uchumi,nishati na usalama. Kansela wa Ujerumani ameisifu Romania kwa  kwa utayari wake wa  kuwapokea wakimbizi wanaomiminika kutoka Ukraine akisema Ujerumani inasimama kwa dhati na Romania.