1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Schröder apinga sheria mpya dhidi ya ugaidi.

13 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFey
COLOGNE: Kansela wa Ujerumani G. Schröder amewaita raiya wawe na tahadhari kubwa kufuatana na orodha hiyo ya mashambulio nchini Uspania. Lakini alisisitiza kuwa wapelelezi wa Kijerumani hawana taarifa zozote kuhusu kitisho cha shambulio la kigaidi nchini Ujerumani, ndiyo maana alisema hakuna haja ya kupitishwa sheria mpya kuhusu mapigano dhidi ya ugaidi. Mashambulio ya umwagaji damu kama yale ya Madrid hayapigwi vita kwa kupitishwa sheria mpya, alisema Kansela, bali kwa kuchukuliwa hatua za kuwasaka watendaji na kuwapa adhabu kali. Kansela Schröder akaendelea kuonya kuwa ugaidi usiambatanishwe kabisa na ule mjadala kuhusu sheria ya uhamiaji.