1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Schröder apinga matumizi ya nguvu dhidi ya Iran

14 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEku

Berlin:

Kansela wa Ujerumani, Gerhard Schröder, ametilia mkazo umuhimu wa kupatikana suluhisho la amani kuhusu mradi wa kinuklia wa Iran. Anapinga pia utumiaji wa nguvu dhidi ya nchi hiyo. Kansela Schröder, akihojiwa leo na gazeti la „Bild am Sonntag“ amesema kuwa kila kitu lazima kifanywe kuhakikisha kuwa mradi wa nishati ya kinuklia wa Iran ni kwa ajili ya matumizi ya amani peke yake. Kansela Schröder amesema kuwa bado ana matumaini kuwa mazungumzo yatafanikiwa ingawaje Iran imekataa mapendekezo ya misaada yaliyotolewa mapema mwezi huu na nchi za Umoja wa Ulaya ili isimamishe mradi wake wa kinuklia. Rais Bush wa Marekani ametishia kuwa haondoi uwezekano wa kutumia nguvu iwapo Iran itakataa kutekeleza miito ya kimataifa ya kusimamisha harakati zake za kinuklia.