Kansela Schröder anautembelea mji wa Kaliningrad,nchini Rashia
3 Julai 2005Matangazo
KALININGRADE:
Kansela Gerhard Schröder amekua kiongozi wa kwanza wa serikali ya Ujerumani kuutembelea mji wa Kaliningrad nchini Rashia.Kansela Schröder amekwenda huko kushiriki katika sherehe za kuundwa mji huo uliokua miliki ya Ujerumani na kujulikana kama Königsberg,miaka 750 iliyopita.Kabla ya kuhudhuria sherehe hizo kansela Schröder anakutana na rais Vladimir Putin wa Rashia na rais Jacques Chirac wa Ufaransa katika mji wa mwambao wa SWETLOGORSK.Mazungumzo yao yatatuwama juu ya mkutano ujkao wa viongozi wa G8 nchini Ireland na mzozo kuhusu mradi wa kinuklea wa Iran.Kabla ya hapo rais Vladimir Putin akifungua sherehe za miaka 750 ya Kaliningrad ,alielezea azma ya nchi yake ya kuendeleza ushirikiano wa dhati pamoja na umoja wa Ulaya.