Kansela Schröder apinga sheria mpya dhidi ya ugaidi.
13 Machi 2004COLOGNE: Kansela wa Ujerumani G. Schröder amewaita Wajerumani wawe na tahadhari kubwa kufuatana na orodha hiyo ya mashambulio nchini Uspania. Lakini alisisitiza kuwa wapelelezik wa Kijerumani hawana taarifa zozote kuhusu kuweko kitisho cha shambulio la kigaidi nchini Ujerumani, ndiyo maana alisema hakuna haja ya kupitishwa sheria mpya kuhusu mapigano dhidi ya ugaidi. Mashambulio ya umwagaji damu kama yale ya Madrid hayapigwi vita kwa kupitishwa sheria mpya, alisema Kansela, bali kwa kuchukuliwa hatua za kuwasaka watendaji na kuwapa adhabu kali. Kansela Schröder akaendelea kusisitiza kuwa uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama ya Katiba ya Ujerumani dhidi ya kupelelezwa nyumba za washutumiwa si kizingiti hata kidogo katika mapigano dhidi ya ugaidi.