1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KANSELA MERKEL ASEMA UGIRIKI NI SEHEMU THABITI YA UMOJA WA EURO .

Abdu Said Mtullya15 Septemba 2011

Ugiriki kuendelea kuwa mwanachama wa Umoja wa Sarafu ya Euro.

https://p.dw.com/p/12ZMv

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa wametamka wazi kwamba Ugiriki licha ya kuwa na madeni makubwa ,itabakia katika Umoja wa sarafu ya Euro.

Wakizungumza na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Giorgis Papandreou katika mkutano uliofanyika kwa njia ya simu, Merkel na Sarkozy walieleza kuwa Ugiriki ni sehemu thabiti ya Umoja wa sarafu ya Euro.

Lakini viongozi hao wameitaka Ugiriki isonge mbele kwa dhati na juhudi za kuutekeleza mpango wa kubana matumizi na kufanya mageuzi. Kansela Merkel na Rais Sarkozy wamesema kwamba hilo ndilo sharti la Ugiriki kuweza kupatiwa fedha zaidi.