Kansela Merkel akutana na Waziri Mkuu wa Italia Prodi
21 Novemba 2007Suala la mustakbali wa Kosovo limehodhi mazungumzo kati ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi hapo jana.
Katika mkutano wao uliofanyika karibu na mji mkuu wa Berlin Merkel ametilia mkazo kuwepo kwa msimamo mmoja wa Umoja wa Ulaya kuhusu suala la jimbo hilo la Serbia.Prodi amesisitiza kuihakikishia serikali ya Serbia kwamba mustakbali wake uko katika Umoja wa Ulaya.Afghansitan pia ilikuwa juu kwenye agenda ambapo viongozi hao wote wawili wametowa wito wa kufanyika kwa mkutano mpya wa kimataifa wa juhudi za ujenzi mpya nchini humo.
Kwa mujibu wa duru za Italia mkutano huo unaweza kuwa na msingi kama ule wa mkutano wa mwaka 2006 mjini London ambao umechangisha euro bilioni 8.7 kwa ujenzi mpya wa Afghanistan.