1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Gerhard Schröder anasema anaamini makubaliano yatafikiwa kuyafuta madeni ya nchi masikini kabisa barani Afrika

7 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEwa

Mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa manane tajiri kwa viwanda umefunguliwa pakiwepo ulinzi mkali huko Gleneagles Scottland.Malkia Elizabeth wa pili wa Uengereza aliwakaribisha viongozi hao kwa karamu ya chakula cha usiku.Mazungumzo yao yaliyoanza rasmi jana usiku,yanahusiana miongoni mwa mengineyo na sera za maendeleo na mazingira.Kansela Gerhard Schröder amesema anaamini makubaliano yatafikiwa ili kufuta madeni ya nchi masikini kabisa barani Afrika.Kansela Gerhard Schröder ,sawa na rais George W. Bush wa Marekani wamezitaka nchi husika za kiafrika zifuate misingi ya tawala zinazoheshimu sheria.Hata katika suala la usafi wa hali ya hewa dalili za maridhiano zimeanza kuchomoza.Duru za Italy zinasema washiriki wamekubaliana juu hatua za kupunguza moshi wa viwandani.Duru hizo hazijataja lakini moshi huo utapunguzwa kwa kiwango gani.