1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Angela Merkel Ziarani mjini Washington

2 Mei 2014

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel yuko ziarani Marekanii. Mara baada ya kuwasili amekutana na maseneta kabla ya kuwa na duru ya kwanza ya mazungumzo pamoja na rais Barack Obama.

https://p.dw.com/p/1BsMS
Kansela Angela Merkel akikamatiwa mlango wa gari na mtumishi wa idara ya usalama alipowasili uwanja wa ndege mjini WashingtonPicha: dpa

Mzozo wa Ukraine, vikwazo dhidi ya Urusi ,kashfa ya shirika la upelelezi la Marekani NSA pamoja pia na makubaliano ya biashara huru kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya ndizo mada kuu zitakazogubika mazungumzo kati ya kansela Angela Merkel na mwenyeji wake-rais Barack Obama mjini Washington.Wadadisi wanaashiria mazungumzo tete kati ya viongozi hao.

Edward Snowden,mtumishi wa zamani wa idara ya upelelezi ya Marekani ameutia sumu uhusiano kati ya Washington na Berlin alipofichua siri za kipeo cha opereshini za upelelezi za idara hiyo ya NSA na hasa kunaswa mawasiliani ya simu ya mkono ya kansela Angela Merkel..

Serikali kuu ya mjini Berlin inataka yafikiwe makubaliano yatakayopiga marufuku mtindo wa kupelelezana,lakini wamarekani wanasita sita.

Kishindo cha kurejesha hali ya kuaminiana

Balozi wa zamani wa Marekani mjini Washingon Wolfgang Ischinger anatoa sababu ya hali hiyo kwa kusema"Kwa bahati mbaya idadi kubwa ya wamarekani bado hawajaelewa madhara yaliyosababishwa na kashfa ya NSA katika jamii ya Ujerumani.Kwa mujibu wa vyombo vya habari sifa ya Marekani kama mshirika imechujuka.Na watu hawawezi kuligeukia suala jengine bila ya kujaribu kwanza kurejesha hali ya kuaminiana.Matarajio ya kuanzishwa mdahalo kuhusu matumizi ya mtandao kaati ya wasahirika ni jambo la maana.Lakini tusitarajie makubwa."

Deutschland Symbolbild Skandal um Spähaktion NSA-Geheimdienst
Picha inayotoa sura ya kipeo cha kashfa ya upelelezi ya idara ya NSA nchini UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Muda mfupi baada ya kuwasili mjini Washington kansela Angela Merkel alikutana na wawakilishi wa baraza la Senet la Marekani.

Awamu ya tatu ya vikwazo dhidi ya Urusi itajadiliwa

Msemaji wa serikali ya Marekani Jay Carney ameshadidia hali nchini Ukraine itagubika mazungumzo.Wabunge wa Marekani wanamtaka kansela Angela Merkel aunge mkono vikwazo vikali dhidi ya Urusi badala ya kufikiria zaidi makampuni ya kiuchumi ya Ujerumani.Hata ikulu ya Marekani kuna wanaopaza sauti kumtaka rais Obama aiwekee vikwazo vikali zaidi Urusi.Wakati wa mazungumzo yao kwa hivyo huenda rais Barack Obama na kansela Angela Merkel wakazungumzia uwezekano wa kuanzishwa awamu ya tatu ya vikwazo hivyo ambayo .Vyombo vya habari vya Marekani vinasema Obama atataka kupata hakikisho kutoka kwa kansela kwamba Berlin itaunga mkono hatua hiyo.

Symbolbild Russland Sanktionen USA Obama
Kitambulisho cha vikwazo dhidi ya Urusi:Picha ya rais Barack Obama akizungumza na kansela Angela Merkel katika mkutano na waandishi habari mjini Berlin Juni 19 mwaka 2013Picha: picture-alliance/dpa

Baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo viongozi hawa wawili wamepangiwa kuzungumza na waandishi habari .Baadae kansela Angela Merkel anapanga kutetea umuhimu wa kufikiwa makubaliano ya biashara huru kati ya Umoja wa ulaya na Marekani na kumalizia ziara ya saa 24 kwa kufanya mazungumzo pamoja na mkuu wa shirika la fedha la kimataifa IMf bibi Christine Lagarde.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/AFP

Mhariri: Josephat Charo