Kansela Angela Merkel na alivyopanda madarakani
29 Oktoba 2018Licha ya juhudi za baadhi ya wanahabari wa kimataifa kutaka kupata hisia zake baada ya kuteuliwa katika wadhifa huo, Angela Merkel alikuwa na wakati mgumu kujieleza wakati wa mkutano wake wa kwanza na wanahabari mwaka 2005. Alipoulizwa anajihisi vipi, alijibu kwamba yuko salama na katika hali nzuri. Jibu lake lilikuwa tu la mwanamke wa kawaida ambaye alijitahidi kupata kazi hiyo yenye hadhi kubwa ya kisiasa nchini Ujerumani kwa kuzingatia siasa kwa upendeleo wa umma.
Merkel hakuchukuliwa kwa uzito kwa muda mrefu na idadi kubwa ya umma. Alizaliwa katika jimbo la Hamburg lakini alikulia eneo la Templin, Kaskazini mwa mji wa Berlin, ambayo ilikuwa ya Kikomunisti, Ujerumani Mashariki. Kwa Merkel, mpaka leo, eneo alikotoka lina umuhimu mkubwa. Merkelv alisomea somo la Fisikia mjini Leipzig na kupata Shahada ya Uzamifu katika Chuo Binafsi cha Sayansi Ujerumani Kaskazini .
Alianza kujihusisha na siasa baada ya kuanguka kwa utawala wa kikomunisti, na kuonekana katika ulingo wa siasa kwa mara ya kwanza kama naibu msemaji wa serikali ya kidemorasia ya Ujerumani Mashariki. Baadaye kazi yake ilianza kushika kasi, ambapo Kansela wa Ujerumani Magharibi Helmut Kohl alimteua kuwa Waziri wa Masuala ya Wanawake na Vijana. Magazeti yalimpa jina ´Msichana wa Kohl´.
Baada ya Kohl kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 1998 na mpinzani wake wa chama cha SPD Gerhard Shröder, Mwenyekiti wa CDU Wolfgang Schaüble alimteua Merkel kuwa Katibu Mkuu wa hama hicho. Wakati kulitokea kashfa ya fedha na Kohls kukana kufanya chochote kibaya, suala lililokiweka chama hicho kwenye shida, Merkel alitakiwa kukianzisha upya kama kiongozi wa CDU.
Mnamo mwaka 2002. Merkel alijiondoa na kumwacha Edmund Stoiber, Mwenyekiti wa hamacha CSU ambacho ni mshirika wa CDU kushindanana Gerhard Schröber katika uchaguzi wa kitaifa. Stoiber alishindwa na kumfanya Merkel kuibuka na ushindi mkubwa. Kando na kuwa kiongozi wa DU; vilevile alichukua wadhifa wa kiongozi kundi la muungano wa CDU na CSU.
Hatua hiyo iliwafanya wapinzani wa Merkel wa ndani ya chama kutambua kuwa yeye ni mpinzani wa kuogopewa.
Mwandishi: Sophia Chinyezi/ /dw/en/chancellor-angela-merkel-and-her-quiet-rise-to-power/a-1600411
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman