Merkel alirejea ofisini mnamo siku ya Ijuma
3 Aprili 2020Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amerejea ofisini kwake siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wiki mbili ziliopita. Kansela huyo wa chama cha kihafidhina cha "CDU" alijiweka karantini baada ya daktari aliempa chanjo kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona siku mbili baadaye.
Hata hivyo kwa mujiibu wa msemaji wa ofisi ya kansela Steffen Seibert, vipimo vilibaini kuwa Merkel hajaambukizwa virusi hivyo hatari. "Tunashukuru kuwa vipimo kadha vimeonyesha kuwa kansela bado hajaambukizwa na virusi vya Corona", Seibert alisema huku akiongeza kuwa, sasa ataendelea kufanyia kazi nyumbani kwake."
Wakati akijitenga nyumbani kwake, Merkel amekuwa akifanya mikutano ya serikali kupitia kwenye njia ya video
Kulingana na utafiti uliofanyika hivi karibuni na shirika la utangazaji la umma nchini humo "ARD" umaarufu wa Merkel umepanda kutoka kwa raia wa Ujerumani, katika kipindi hiki cha janga la virusi vya Corona, wengi wao wakiridhishwa na hatua zilizochukuliwa.
Kwa mujiibu wa utafiti huo, asilimia 88% ya raia nchini humo wanaridhishwa na hatua za chama chake Merkel "CDU" za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya hivyo hatari. Serikali ya shirikisho ya Ujerumani imetoa mikakati kadhaa ikiwemo kuwataka watu kutokaribiana mno na kuzuia mikusanyiko ya watu wengi kama mojawapo ya kuzuia kupanda kwa mambukizi ya Corona.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni za chuo kikuu cha Johns Hopkins watu wapatao 1,107 wamefariki kutokana na virusi vya Corona na wengine 84,794 kuambukizwa nchini Ujerumani.
Chanzo: DW