Kanisa Katoliki nchini Kenya limeanza kampeni kuupinga mpango wa serikali wa kuanzisha mafunzo ya uzazi mashuleni kwenye mtaala mpya unaotekelezwa. Kanisa hilo linahofia kuna mambo hayajawekwa wazi hivyo wanautilia shaka mchakato mzima. Mashirika ya kijamii hata hivyo yana mtazamo tofauti, yakisema mpango huo utayakabili maambukizi ya magonjwa ya zinaa kati ya vijana pamoja na mimba za mapema.