1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kandanda:Timu ya kandanda ya Schalke imebakia inaoongoza hadi jana katika ligi ya Ujerumani, ikitoka sare mabao mawili kwa mawili na Wolsburg.

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRC

Timu inayoinyemelea kwa karibu Schalke, nayo ni Bremen ilibwagwa nyumbani na Hamburg kwa mabao mawili kwa bila. Katika mashindano mengine ya jana, Aachen iliikanyaga Bayern Munich bao moja kwa bila; Leverkusen ikapoteza pointi tatu kwa kushindwa bao moja kwa bila na Hannover; Dortmund iliicharaza Mönchengladbach bao moja kwa bila; Hertha Berlin ilinyolewa nyumbani na Mainz kwa mabao mawili kwa moja. Leo jioni Bielefeld inapambana na Bochum na Nuremberg itamenyana na Energie Cottbus.