1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kandanda: Timu za kabumbu za Borussia Dortmund na Schalke za hapa...

28 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxD
Ujerumani zimetolewa katika mashindano ya kuwania Kombe la UEFA la Shirikisho la kabumbu la Ulaya. Schalke ilibandikwa mabao mawili kwa moja na Klabu ya Brondby huko Copenhagen, Denmark. Hivyo klabu hizo mbili zikawa na mabao sawa, lakini baadae Schlake ilishindwa katika michuano ya mikwaju ya penalty mwisho wa mchezo wa jana usiku. Katika mechi nyingine, klabu ya Ufaransa ya Sochaux Soundly iliibwaga Borussia Dortmund mabao manne kwa bila. Na mchezaji wa kandanda wa Kiengereza, David Becham, ametunukiwa nishani ya OBE na Malkia Elizabeth wa nchi yake. Alikabidhiwa nishani hiyo na malkia katika Kasri la Buchingham.