1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kandanda kuchezwa kwa dakika 60?

19 Juni 2017

Jopo linalotunga sheria za kandanda linataka mjadala uanzishwe kuhusu pendekezo tata la kupunguza muda wa mchezo wa kandanda kutoka dakika 90 hadi 60 na kusimamisha saa wakati mpira umesimamishwa

https://p.dw.com/p/2exCz
Brasilien FIFA Confederations Cup Howard Webb
Picha: Getty Images/AFP/Y. Cortez

Bodi ya  Kimataifa ya Kandanda – IFAB inasema kuwa kama mpira utachezwa kwa dakika 30 katika kila kipindi yatakuwa ni mabadiliko makubwa kwa sheria za kandanda. Hayo tu ni miongoni mwa nakala ya mkakati wa miaka mitano wa mada za kujadiliwa na mapendekezo ikiwa na malengo matatu: kuongeza heshima, muda wa kucheza na mvuto wa mchezo.

Wakosaoji wanasema kuwa mabadiliko kama hayo hayatakuwa na umuhimu wowote kama sheria ya kupoteza muda haitaimarishwa. Mapendekezo mengine ni pamoja na kuweka saa kubwa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira ama hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu

Mabadiliko yoyote huenda yakachukua miaka mingi ya majaribio kabla ya kuidhinishwa na majaribio yatakayosimamiwa na IFAB, bodi inayotathmini sheria za kandanda kila mwaka na inajumuisha maafisa kutoka FIFA na vyama vinne vya kandanda vya Uingereza.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Josephat Charo