KANDAHAR Uhispania kupeleka wanajeshi zaidi nchini Afghanistan
23 Juni 2005Matangazo
Uhispania imeahidi kuwapeleka wanajeshi wake 500 kwenda Afghanistan mwanzoni mwa mwezi Julai kusaidia kuandaa uchaguzi wa bunge. Waziri wa ulinzi wa Uhispania, Jose Bono, amesema wanajeshi hao watakuwa nchini humo kwa miezi mitatu.
Nchini Afghanistan, wanajeshi wa Marekani na wa Afghanistan wamewaua wanamgambo zaidi ya 70 wa kundi la taliban kusini magharibi mwa nchi hiyo. Duru za jeshi la Marekani zinasema walinda usalama wanane waliuwawa katika opresheni hiyo na wapiganaji zaidi ya 30 wamekamatwa. Opresheni hiyo inalenga kuwachakaza wanamgambo kabla uchaguzi kufanyika mwezi Septemba.