KANDAHAR : Ndege ya NATO yaanguka
2 Septemba 2006Matangazo
Ndege ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO imeanguka leo hii kusini mwa Afghanistan kutokana na hitilafu ya kiufundi lakini hakuna habari zilizoweza kupatikana mara moja juu ya maafa.
Msemaji wa majeshi ya muungano nchini humo Meja Quentin Innis amesema bila ya kutowa ufafanuzi zaidi kutokana na wasi wasi wa kiusalama kwamba kuanguka kwa ndege hiyo hakuhusiani na kitendo cha adui.
Amesema ndege hiyo imeanguka wakati wa operesheni katika Panjwayi kusini mwa jimbo la Kandahar ambapo mamia ya wanajeshi wa NATO na wale wa Afghanistan wameanzisha shambulio kubwa dhidi ya waasi wa Taliban leo hii.