KANDAHAR: Mlolongo wa magari ya NATO umelengwa na mshambuliaji
3 Desemba 2006Matangazo
Hadi watu 8 wameuawa katika mji wa Kandahar kusini mwa Afghanistan,baada ya mshambuliaji aliejitolea muhanga,kujaribu kuliendesha gari lake liliokuwa na bomu dhidi ya mlolongo wa magari ya vikosi vya NATO.Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari,wanajeshi upesi walifyatua risasi zilizowapata watu,ndani ya magari yao na kuwajeruhi raia wengine wa Kiafghanistan. Haijulikani ni idadi gani walijeruhiwa na mripuko wa bomu na wangapi kwa risasi za wanajeshi. Mripuko huo wa bomu uliwajeruhi vile vile wanajeshi 3 wa NATO.