1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya umeme ya Ghana yalikatia umeme bunge

1 Machi 2024

Kampuni ya usambazaji umeme inayomilikiwa na serikali ya Ghana( ECG) imelikatia umeme bunge la taifa hilo kama hatua ya kulishinikiza kulipa deni la dola milioni 1.8.

https://p.dw.com/p/4d4DB
Bunge la Ghana
Bunge la Ghana likiendelea na vikao vyake. Picha: Isaac Kaledzi/DW

Tukio hilo la siku ya Alhamis (Februari 29) lilivuruga mjadala bungeni

Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo, William Boateng, alithibitishia shirika la habari la Reuters kuwa kampuni yake iliamua kukata umeme baada ya bunge kushindwa kutimiza ahadi ya kulipa deni lake.

Soma zaidi: Uchaguzi wa Ghana 2020 ni kushindwa kwa Demokrasia

Hata hivyo, umeme ulirudishwa muda mfupi baadaye baada ya bunge hilo kulipa dola milioni moja na kuahidi kulipa fedha nyingine haraka iwezekanavyo.