1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pfizer imetangaza kidonge cha kupunguza makali ya Covid-19

6 Novemba 2021

Kampuni ya madawa ya Pfizer imesema jaribio la kidonge chake cha kutibu ugonjwa wa Covid-19 limeonesha kuwa kinaweza kupunguza makali ya uwezekano wa mgonjwa kulazwa hospitali au kufa kwa asilimia 89.

https://p.dw.com/p/42etv
Molnupiravir
Picha: Merck & Co Inc/REUTERS

Kwa mujibu wa taarifa ya jana, Ijumaa ya kampuni hiyo, jaribio hilo linawahusu hasa watu wazima ambao wapo katika hatari ya kuathiriwa vibaya na virusi hivyo, kwa kusema tiba hiyo itakuwa silaha mpya dhidi ya janga la virusi vya corona.

Jaribio hili la sasa linaonesha kuwa la mafanikio zaidi ikilinganishwa na dawa ya kampuni ya Merck & Inc's pill, molmupiravir ambayoo mwezi uliopita ilionesha kinapunguza kwa kiwango cha nusu ya hatari ya kufa au mgonjwa kufikia katika hali ya umaututi.

Kidonge kipya kwa ajili ya Covid-19 kitaitwa Paxlovid

Symbolbild Impfstoff Impfung Coronavirus
Nembo yenye kuwakilisha makampuni Biontech&PfitzerPicha: FrankHoemann/SvenSimon/picture alliance

Kidonge cha Pfizer, ambacho kimepewa jina la chapa ya Paxlovid, kinatarajiwa kupata idhini ya mamlaka ya udhibiti ya Marekani, katika kipindi cha mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuanza kutumiwa. Inaelezwa jaribio la dawa awali lilisitishwa kutokana na kiwango kikubwa cha kuonesha bmafanikio.

Hata hivyo, data za jaribio kamili za hatua hiyo bado kutoka kwa kampuni zote mbili. Tayari Rais wa Marekani Joe Biden ameonesha nia ya kudhibiti mamilioni ya dozi ya dawa hiyo kwa ajili ya raia wa taifa lake. Kiongozi huyo amenukuliwa akisema kama itaridhiwa na Mamala ya Chakula na Dawa ya Marekani FDA kwa haraka sana tutaanza kuitumia dawa hiyom kuwatibu wale wote waliopata maambukizi.

Pamoja na uvumbuzi huo lakini chanjo ni bado itasalia kinga bora

Vidonge hivyo vitaambatanishwa na vidonge vingine vya kukabiliana na virusi vya zamani viitwavyo ritonavir. Tiba yake itahusisha vidonge vitatu ambavyo ambavyo mtumiaji atapaswa kumeza mara mbili kwa siku. Jitahada hiyo ya kimaabara imetumia takribani miaka miwili.

Pamoja na kuonesha uwezo, kunakolezwa na makampuni ya Pfizerna Merck, kwamba kidonge kinaweza kudhibiti maambukizi ya Covid-19 kwa matumizi yake lakini bado chanjo inasalia kuwa njia bora zaidi kudhibi janga la virusi vya corona ambalo limewauwa zaidi ya milioni 5 duniani kote, ikiwa ni pamoja na watu zaidi ya 750,000 kwa Marekani pekee.

Chanzo: RTR