Kampuni ya magari ya Tata ya India yanunuwa kampuni za magari za Jaguar na Land Rover nchini Uingereza
28 Machi 2008Kampuni ya magari ya Marekani Ford ikanunuwa kampuni hizo mbili za magari ya kifahari miaka kadhaa iliopita.Tatizo la kutambulikana kwa jina la Ford lilikuwa kubwa mno kwamba mara mbili kundi la makampuni linalounda shirika hilo la magari la Marekani lilifikia ukingoni mwa kufilisika na hiyo kupoteza utashi kwa makampuni ya shirika la magari barani Ulaya yenye majina makubwa.
Hivi sasa kampuni ya Tata ya India imenunuwa kampuni za magari aina ya Jaguar na Land Rover za Uingereza.
Watu wanaohusudu magari nchini Uingereza yumkini wakawa na hisia mchanganyiko.Kundi la makampuni linalounda shirika la magari la India Tata kwa mara ya kwanza kabisa limechangamkia biashara ya magari kwa kufikia hatua ya kununuwa kampuni mbili mashuhuri za magari nchini Uingereza za Jaguar na Land Rover.
Mmiliki wa muda mrefu wa kampuni hiyo yaani kampuni ya magari ya Marekani Ford imekuwa na mazungumzo ya takriban mwaka mmoja na makundi husika.Hivi sasa makubaliano yao yamekamilika.Euro bilioni moja na nusu zimetumbukizwa kwenye makubaliano hayo.Halafu kampuni ya Ford italazimika kuzipatia kampuni hizo mbili kila moja bilioni mbili na nusu kwa mwaka.
Jaguar italipwa fedha hizo kwa kipindi cha miaka 19 wakati Land Rover italipwa kwa miaka minane.
Hata hivyo kwa sasa mkuu wa shirika la magari la Tata Ravi Kant hana dhana kwamba kampuni yake hiyo itakuwa ya kimataifa. Katika maonyesho ya magari ya Genfer Autosalon huko Geneva alitangaza mkakati wa kujitanuwa kwa kampuni hiyo.
Amesema anailenga Thailand,Indonesia na maeneo kama hayo pia wanaziangalia nchi kadhaa za Kiafrika,Amerika ya Kusini na wanahisi kwamba wana nyenzo ya uhakika kwa kule kumiliki kampuni hizo mbili kuu za magari za Uingreza Jaguar na Ford ambazo majina yake yanatambulikana na yana umuhimu mkubwa wa kimataifa.
Kampuni ya Jaguar hadi hii leo inaendelea kuwa kampuni maalum ya kuwapatia magari Malkia na Prince Charles wa Uingereza.Lakini Ford haiwezi kujifariji kutokana na kutumbukia kwenye hasara. Kinyume chake kampuni ya Land Rover ilikuwa na maendeleo mazuri katika miaka iliopita.Katika kampuni hizo mbili kuna wafanyakazi zaidi ya 15,000 walioajriwa nchini Uingereza.Juu ya kwamba mustakbali wao sio wa uhakika wafanyakazi hao wako furahani.
John Reed mwandishi wa habari wa masuala ya fedha mjini Londo anasema hadhani kwamba wataweza kupunguza nafasi za ajira katika kipindi cha muda mfupi na atashanga sana iwapo wataweza kufanya hivyo kwani wafanyakazi wao wana hakikisho la ajira la miaka mitano.Anasema pia kuna wafanyakazi wa kupindukia kwenye viwanda vyake vitatu ambavyo hutengeneza magari kama 300,000 hivi kwa mwaka.Reed anaona nafasi za ajira itabidi zipunguzwe katika kipindi cha kati au baadae sana.
Vyombo vya habari vya masuala ya fedha nchini Uingedreza vinaona uuzaji wa kampuni hizo ni hatua ya mkakati na wachezaji wapya katika meza ya mashirika ya magari. Tata itakuwa inaingiza miguu yake kwenye soko la ushindani barani Ulaya na Ford lazima ishughulikie hasara inayosumbuwa kichwa chake.
Hayo ni maoni ya Jay Nagley mchambuzi wa masuala ya hisa mjini London ambaye anasema wanataka kutimiza dhima kubwa duniani na kwamba tayari wana nguvu za kutosha na magari yanayofaa huko Asia na hivi sasa wameanzisha gari la gharama nafuu kabisa duniani ambalo nchini India linajulikana kama Tata lakini ili waweze kuwa na dhima katika ngazi ya dunia inabidi wawe na nguvu barani Ulaya na kwa kuwa hawana biadhaa kutoka India zitakazowaweka kwenye nafasi hiyo kwa hiyo imebidi wanunuwe kampuni ya Ulaya yenye jina linalotambulikana la hadhi kubwa duniani.
Mashirika mashuhuri ya magari yaliojitengenezea majina nchini Uingereza yana uzoefu tafauti na wadau wa kigeni. Ndoa ya muda mfupi kati ya kampuni ya BMW na Rover haikuwacha kumbukumbu nzuri lakini kwa vyo vyote vile wafanyakazi wa kampuni zote mbili za Jaguar na Land Rover wana matumaini kwamba hali haitokuwa mbaya sana na mmiliki wao mpya kuipindukia ile iliopita.