Kampuni ya Bavarian Nordic kutengeneza dozi 440,000 ya mpox
22 Agosti 2024Matangazo
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Paul Chaplin amesema maombi ya kusambaza dozi hizo za chanjo yalijumuishwa kwenye makadirio yake ya mwaka huu.
Wiki iliyopita, kampuni hiyo ilisema iko tayari kutengeneza chanjo hadi dozi milioni 10 ya mpox ifikapo mwisho wa mwaka 2025.
Shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa kutengenezwa kwa chanjo zaidi huku kipaumbele ikiwa kwa nchi zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo wa homa ya nyani.
Soma pia: Tanzania yaanza ufuatiliaji ili kuzuia maambukizi ya Mpox
Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, kimeeleza kuwa dozi 20,000 za chanjo zitasambazwa kote barani Afrika, kufuatia makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na kampuni ya kutengeneza dawa ya Bavarian Nordic.