SiasaChad
Kampeni za kura ya maoni itakayofanyika Desemba zaanza Chad
25 Novemba 2023Matangazo
Zoezi hilo litakuwa kipimo cha uhalali wa serikali ya kijeshi na utawala wa kiimla wa familila ya Deby Itno uliodumu kwa miaka 30.
Zaidi ya watu milioni 8.3 katika nchi hiyo kubwa lakini maskini ya ukanda wa Sahel, wanatazamiwa kushiriki kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Desemba 17, ikiwa pia ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu na kurejesha utawala wa kiraia.
Rais wa mpito wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye uongozi wake wa kijeshi umetawala tangu mwaka 2021, aliahidi kukabidhi madaraka kwa raia na kufanya uchaguzi mwaka huu kabla ya kuuahirisha hadi mwaka 2024.