Kampeni ya siku 16 kupinga ukatili dhidi ya wanawake Burundi
25 Novemba 2020Serikali ya nchi hiyotayari imeunda kamati hadi kwenye ngazi ya tarafa za kuwatega sikio wanawake wanaokumbwa na masaibu hayo.
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za wanawake Giriteka wanawake elf 13 133 walikabiliwa na visa vya kudhalilishwa kijinsia mwaka jana. Mikoa ya Gitega, Ruyigi, Muyinga na Ngozi ikionekana kuongoza kwa idadi kubwa ya visa hivyo.
Mkuu wa shirika Giriteka la kutetea haki za wanawake Bi Jeanne Gacoreke anaye tambulika kwenye Umoja wa Mataifa kama mmoja ya wanaharakati wa haki za wanawake anasema migogoro isiyokoma, mila potofu na hata umasikini ni sababu kubwa zinazochangia katika kadhia hiyo ya unyanyasaji wa kingono.
Kimataifa: Vita dhidi ya ukatili kwa wanawake
Katika mji mkuu Bujumbura hali imeonekana kuanza kuboreka ambapo idadi ya visa vya unyanyasaji kijinsia imeonekana kupunguwa limesema shirika hilo la Giriteka.
kwa upande wake serikali ya Burundi putia waziri anaye husika na haki za binaadam na mshikamano kitaifa, Imelde Sabushimike amesema serikali inaielewa hali hiyo ndio sababu zilibuniwa kamati hadi kwenye ngazi ya kitarafa za kuwatega sikio wanawake, ili hatimaye kuhakikisha visa hivyo vimekomeshwa.
Juhudi za kila mmoja kukomesha ukatili dhidi ya wanawake
Mada ya mwaka huu ni mchango wa kila mmoja katika kutokomeza visa vya kumnyanyasa mwanamke inaonesha wazi jukumu la kila raia. Ndio sababu serikali tayari imeunda kamati za kusikiliza malalamiko na mapendekezo ya wanawake ili hatimaye unyanyasaji kijinsia ukomeshwe nchini.
Tanzania: Wito watolewa wa kukomesha unyanyasaji wa ngono
Mkuu wa shirika la Giriteka anasema Licha ya uwezo mdogo katika kuwasaidia wahanga wa visa vya unyanyasaji kijisia, mashirika ya kutetea haki za wanawake yamekuwa yakiendesha harakati za kuhamasisha raia na hususan wana ndoa ili kuhakikisha visa hivyo havitokei tena katika miaka ijayo.
Kwenye shughuli za siku hizi 16 za kupambana na Unyanyasaji mwanamke kijinsia, mkuu wa shirika la Giriteka Jeanne Gacoreke anaye tambulika kama moja ya wanawake 1000 duniani katika harakati za wanawake, anasema wanawake wanaoishi na ulemavu wa kutosikia huonekana kusahaulika.
Wakati ambapo ni tabaka ya wanawake wanao sibiwa zaidi na visa vya kunyanyaswa kijinsia. Na kwamba wakati huu ulimwengu wakabiliwa na Covid 19 wengi wao nchini hawajui kinacho endelea juu ya janga hilo.