1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni juu ya mabadiliko ya hali ya hewa

Lillian Urio27 Juni 2005

Wakati wa mkutano wa nchini wanachama wa G8 mwezi ujao, kengele zitagongwa kama ishara kwa viongozi wa dunia iliwachukue hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

https://p.dw.com/p/CHgD

Chama cha kimataifa cha kulinda mazingira, Friends of the Earth, yaani marafiki wa dunia, wameomba watu duniani kote kupiga kengele ifikapo saa nane kasorobo, mwezi Julai tarehe 7. Mktutano huo wa G8 utafanyika kwenye mji wa Gleneagles, huko Scotland.

Friends of the Earth wamechagua saa nane kasorobo kwa sababu katika masaa ya ishirina na nne, ni saa kumi na tati na dakika arobaini na tano. Wamesema nchi wanachama wa G8, wana asilimia kumi na tatu ya watu duniani kote lakini wanatoa asilimia 45 ya gesi zinazoharibu ulimwengu.

Gesi hizo ambazo kimsingi ni za dioksidi za kaboni na methani zinaongeza joto kwenye angahewa na hii hubadilisha hali ya hewa na kusababisha matatizo makubwa ya kimazingira, kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Duncan McLaren afisa mtendaji wa Friends of the Earth huko Scotland, ameliambia shirika la habari la IPS kwamba mikutano ya G8 imekuwa ikifanyakia kwenye maeneo ambayo sio rahisi kwa watu kuyafikia.

Kutakuwa na vizuizi vya watu kufanya maandamanop wakati wa mkutano utakaofanyika Gleneagles. Pia hawataweza kufikia mahala mkutano huo unapofanyika. Hivyo, tendo la kugonga kengele utakuwa ujumbe muhimu kwa washiriki wa mkutano huo na utawafikia.

Bwana McLaren ameeleza kwamba kutoweza kufikia mikutano imekuwa tatizo kubwa kwa watu ambao wanaona hawana uwezo wa kuleta mabadiliko, lakini wangependa kuona mabadiliko yanafanyika.

Ingawa kufanya hivyo sio jambo kubwa, lakini wanaona kwamba wakiwa wengi wanaweza kuisaidia dunia na matukio yatakayotokea kutokanan na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kuna uwezekano kwamba viongozi wa G8, kutoka Uingereza, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Urusi na Marekani, hawatasikia kengele hizo kwenye sehemu ya mkutano wao huko Gleneagles. Lakini watu wengi duniani watasikia kelele za kengele hizo, kutokana wirto wa chama cha Friends of the Earth.

Viongozi hao wa G8 watajua baadhi ya watakao piga kengele. Likiwemo Kanisa la Scotland, hii inamaanisha kwamba kengele zinaweza kupigwa kutoka mji mdogo wa Auchterarder, jirani na hoteli ya Gleneagles sehemu ambayo mkutano unatafanyika mwezi Julai, tarehe 6 hadi 8.

Mapema mwezi huu, Kanisa la Scotland liliamua kushiriki katika mkutano mkuu uliofanyika kwenye mji mkuu wa Scotland, Edinburgh. Na haswa watawasiliana na kanisa la Auchterarder.

Mikutano kadhaa imepangwa kufanyika kwenye kanisa hilo. Lengo ni kuwafikishia viongozi wa G8 ujumbe kwamba wanatakiwa kuwajibika na suala la mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini.

Meena Raman, mwenyekiti wa Friends of the Earth amesema viongozi wa G8 watabaki Glenegleas, katika sehemu ya mkutano. Lakini wao wanaweza kuhakikisha viongozi hao wanasikia matakwa yao. Amewataka watu wengine waungane nao na kuwajulisha viongozi wa dunia kwamba itawabidi wawajibike na matatizo wanayosababisha.

Mjini London, Kanisa kuu la dayosisi Mtakatifu Paulo, ambalo ni kanisa muhimu kwa Kanisa la Uingereza, pia litapiga kengele wakati huo. Hii itakuwa ishara muhimu ya kuonyesha kwamba wanamazingira hao wanaungwa mkono na wakristo.

Chama hicho kinawawezesha watu kugonga kengele kwa kujiandikisha kwenye mtandao, uliotengenezwa kwa ajili hii, wa www.climatealarm.org.

Kwa mujibu wa Friends of the Earth kampeni hii inaungwa mkono na baadhi ya makundi ya makanisa, vyama vya kijamii na wanamazingira duniani kote. Kundi la Islamic Relief limetoa wito wa sala kuendeshwa katika misikiti kwa wakati huo.

Bwana McLaren amesema kwambwa shughuli nyingi zinafanyika katika nchi wanachama wa G8, lakini watu wengi kutoka Brazil, Slovakia, nchi zilizo Afrika, Peru, Argentina, Hong Kong na wa nchi nyingine wanaitikia wito.