KAMPALA:Waasi wa LRA wawasili Kampala bila ya hofu
1 Novemba 2007Matangazo
Wawakilishi wa kundi la waasi wa LRA wamewasili karibu na mji wa Kampala kwa mara ya kwanza bila ya kuwa na hofu juu ya kukamatwa.
Wawakilishi hao wanaandamana na wapatanishi kutoka kwenye mazungumzo yanayofanyika kusini mwa Sudan.
Mazungumzo hayo ni juu ya kusuluhisha mgogoro wa kaskazini mwa Uganda baina ya majeshi ya serikali na waasi hao.