KAMPALA:Waasi wa LRA watakiwa kusalimu amri au kukabiliwa na MONUC
25 Septemba 2005Waasi wa jeshi la Uganda wa LRA waliokimbilia kwenye misitu ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wametakiwa wasalimu amri au warejeshwe nchini Uganda.
Kwa mujibu wa jeshi la Uganda naibu kiongozi wa LRA Vincent Otti aliomba hifadhi ya kisiasa nchini Kongo wiki iliyopita baada ya kuondoka mafichoni kusini mwa Sudan.
Waasi hao wametakiwa wasalimu amri na kukubali msamaha wa serikali ya au wakubali kuhamishwa kwenye nchi ya tatu la sivyo watakabiliwa na jeshi la MONUC.
Duru za serikali ya Uganda zimearifu kwamba maofisa wa Congo, na maafisa wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUC wako kwenye mji wa mpakani wa Aba kukutana na waasi hao.
Lakini waziri wa habari wa Kongo Henri Mova Sakanyi awali alisema kwamba hana habari yoyote kuhusiana na kuingia Congo waasi hao.