1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Rais Museveni atoa onyo kwa waasi wa LRA

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCO7

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameonya kwamba ataanzisha mashambulio mapya dhidi ya waasi wa LRA baada ya kumalizika hii leo kwa muda wa kusimamisha vita endapo waasi hao watakuwepo katika ardhi ya nchi yake.

Waasi wa LRA wamesema hawatarefusha muda huo uliokuwa umewekwa kwa ajili ya kufanyika mazungumzo ya amani kati yake na serikali kuanzia mwezi Juli mwaka jana.

Inaaminika kwamba baadhi ya waasi hao na viongozi wao wamejificha katika sehemu za kusini mwa Sudan na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo huku wengine wakisemekana kuelekea katika jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa upande mwingine naibu kamanda wa LRA Vincet Otti amelishutumu jeshi la Uganda kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha vita kwa kuwashambulia wapiganaji wake kusini mwa Sudan wiki za hivi karibuni na kuapa kulipiza kisasi.