1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Wito wa msaada wa fedha

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNk

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanahitaji pesa kusaidia watu walioathirika vibaya na mafuriko katika nchi nyingi za Afrika. Mashirika hayo yanahitaji zaidi ya Euro milioni 30 kwa ajili ya Uganda peke yake,ambako watu 50 wamepoteza maisha yao na zaidi ya watu 300,000 hawana maji yalio safi.Serikali ya Uganda imetangaza hali ya dharura kwa sababu ya maafa hayo.

Chama cha Msalaba Mwekundu kimepeleka Ghana,Togo na Uganda wataalamu wake kushughulikia misaada ya dharura.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,kiasi ya watu milioni moja na nusu wameathirika na mafuriko,kuanzia Kenya upande wa mashariki hadi Senegal,katika eneo la magharibi.

Wasaidizi wanasema,chakula kitapaswa kupelekwa kwa ndege katika maeneo yaliyopoteza mazao na yametengwa kwa maji.