1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Wajumbe wa LRA watoka nje ya mkutano

10 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDN1

Waasi wa kundi la LRA nchini Uganda walitoka nje ya mazungumzo kati yao na wajumbe wa serikali wakiitaka serikali itangaze usitishwaji wa mapigano.

Kundi la LRA lilitangaza kusitishwa kwa mapigano wiki iliyopita na kuitaka serikali pia ifanye hivyo katika juhudi za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uganda.

Hata hivyo serikali ilikataa ikisema kundi la LRA lingetumia usitishwaji wa mapigano kujikusanya na kujihami na silaha.

Msemaji wa LRA pia amewalaumu wanajeshi wa serikali ya Uganda kwa kuwaua wapiganaji wake wanane tangu waasi hao walipomaliza mapigano.