KAMPALA: Waasi wa LRA wavuka mto Nile
15 Septemba 2005Matangazo
Habari zinasema, waasi wa Uganda kwa mara ya kwanza wamevuka mto Nile na kushambulia sehemu iliyopo katika barabara kuu karibu na mji mkuu wa kusini mwa Sudan Juba.
Waasi zaidi ya 40 wa kundi la LRA walichoma nyumba katika sehemu hiyo wakati wa mchana.
Tokea ghasia zilizofuatia kifo cha kiongozi wa Sudan ya kusini hayati John Garang, barabara hiyo imekuwa kiunganisho muhimu cha mawasiliano kwa mji wa Juba
.