KAMPALA : Waasi wa LRA wadai ICC iwafutie mashtaka
7 Julai 2007Kundi la waasi wa Uganda la LRA hapo jana limeitaka Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kubatilisha mashtaka ya uhalifu dhidi ya viongozi wake waandamizi na kuonya kwamba watazuwiya kufikiwa kwa mkataba wa mwisho wa amani na serikali.
Wiki moja baada ya LRA na serikali ya Uganda kufikia makubaliano ya sheria na usuluhishi msemaji wa waasi Godfrey Ayoo amepa kwamba waasi watayadharau makubaliano ya amani iwapo mashtaka hayo hayatofutwa.
Ayoo ameliamnbia shirika la habari la AFP mji Juba mji mkuu wa Sudan ya Kusini kwamba Mahkama hiyo ya ICC inaendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa amani nchini Uganda na kwamba venginevyo suala hilo linapatiwa ufumbuzi hakuna askari wao wakataotoka kichakani na serikali inapaswa kusahao juu ya utiaji saini wowote ule.