Kampala: Mazungumzo kati ya serikali ya DRC na M23 yaendelea
9 Aprili 2013Matangazo
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 ambayo yalikuwa yamesitishwa kwa kipindi cha wiki tatu yamerejelewa tena mjini Kampala.
Kwenye kikao cha kufungua awamu ya tatu ya mazungumzo hayo, ujumbe wa serikali ya Kinshasa ulisema njia ya kipekee ya kuhakikisha kuwa waasi wa M23 hawatashambuliwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ni kwa kuhakikisha kuwa mazungumzo yanafanikishwa. Mwandishi wetu wa Kampala leylah Ndinda na taarifa zaidi.
Insert
Mwandishi Leyla Ndinda
Mhariri Josephat Charo