1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMESHLI:Polisi wayatibua maandamano ya wakurdi Syria

6 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6W

Polisi nchini Syria wameyavunja maandamano yalikuwa yakifanywa na mamia ya Wakurdi wa nchi hiyo katika mji wa Kaskazini mashariki wa Kameshli.

Hali ya wasiwasi imeongezeka katika mji huo tangu kufanyika maziko ya kiongozi wa kidini wa kikurdi wiki iliyopita.

Maandamano hayo yalipangwa na Vyama viwili vya Kikurdi vilivyopigwa marufuku vikitaka uchunguzi ufanyike juu ya mauaji ya Sheikh Mohammad Maashouq Al Khaznawi.

Serikali ya Syria imetangaza imewakamata watu wawili na kuwastaki kwa makosa ya kumteka nyara kiongozi huyo mwenye msimamo wa kadri wa kidini na ambaye hakuipinga serikali.