Tabia ya kuweka dau kwenye mechi za vilabu vya soka duniani sasa imekuwa biashara kubwa nchini Kenya, ambako inaratibiwa kama kamari nyengine za kawaida, ikizungusha mamilioni ya shilingi kila msimu wa ligi unapowadia. John Marwa anaangalia namna kamari hii inavyozama kwenye maisha ya wakaazi wa mji wa Kisumu.