1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mkutano wa Munich: Harris kuongoza ujumbe wa Marekani

10 Februari 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ataongoza ujumbe wa taifa hilo kwenye mkutano wa mwaka wa masuala ya usalama wa Munich nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4cFTG
 Kamala Harris akiwasili mjini London
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala HarrisPicha: Kirsty Wigglesworth/AP Photo/picture alliance

Hii ni katika wakati ambapo misaada ya kiulinzi kwa ajili ya Ukraine na Israel ikiwa imekwamishwa na bunge la nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliyemalza ziara yake ya Mashariki ya Kati pia atahudhuria kongamano hilo la wiki ijayo linalowakutanisha wanadiplomasia wa magharibi na  maafisa wa kijeshi.

Kulingana na Ikulu ya White House, Harris atatoa hotuba muhimu ya sera ya nje na kufanya mikutano kadhaa na viongozi wa kigeni, kuanzia Februari 15 hadi 17, na kujadiliana kuhusua msaada kwa Ukraine inayopambana na Urusi na hali katika Ukanda wa Mashariki ya Kati.

Kila mwaka kongamano hilo la Munich huwakusanya maafisa wa kijeshi kutoka kote ulimwenguni na huchukuliwa kama kipimo cha mahusiano baina ya Ulaya na Marekani.