Rais wa Rwanda, Paul Kagame amechukua Uenyekiti wa Umoja wa Afrika. Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais wa Guinea, Alpha Conde, baada ya kuchaguliwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwaka jana. Mchambuzi wa masuala ya siasa Dokta Marcos Albanie aliyeko Tanzania anachambua changamoto anazokabiliwa nazo anapochukua hatamu ya kuongoza taasisi hiyo.