Kagame aapishwa, asema amani ya kanda ni 'kipaumbele' chake
12 Agosti 2024Kagame alishinda uchaguzi wa mwezi uliyopita kwa asilimia 99.18 ya kura, na kumpa muhula mwingine wa miaka mitano madarakani.
Wakuu kadhaa wa mataifa na wageni wengine kutoka mataifa ya Afrika walijiunga kwenye sherehe hiyo ya uapisho iliyofanyika mjini Kigali.
Matokeo ya uchaguzi wa Julai 15 hayakuwa na mashaka yoyote kwa Kagame, ambaye amelitawala taifa hilo dogo kwa mkono wa chuma, tangu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, kama kiongozi wa nyuma ya pazia na kisha rais.
Soma pia:Paul Kagame: Shujaa au Dikteta?
Kagame amesema amani ya kanda ndiyo kipaumbele cha Rwanda, lakini haiwezi kuletwa na yeyote au kutoka kokote hata wawe na nguvu kiasi gani, endapo upande unaohusika zaidi haujafanya kinachohitajika.
Rais wa Angola Joao Lounreco, akiwa miongoni mwa waliohudhuria sherehe ya Jumapili, alitarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha na Kagame, kuhusu mpango wa kusitisha vita DRC uliofikiwa wiki iliyopita.