1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabumbu la Ulaya lazama katika bahari ya matapeli

Oumilkher Hamidou23 Novemba 2009

Visa vya udanganyifu katika dfimba vyafichuliwa

https://p.dw.com/p/KdMY
Vyombo vya sheria vyapania kuwaandama matapeli katika kabumbuPicha: picture-alliance/ dpa

Kashfa inayoligubika dimba barani Ulaya ,shirika la usafiri wa reli la Ujerumani Deutsche Bahn lajipatia kandarasi ya kujenga njiya ya reli Qatar na makadirio ya maoni ya umma,nusu mwaka kabla ya uchaguzi katika jimbo hili la North Rhine Westphalia ni miongoni mwa mada zilizomulikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanze lakini na kashfa ya bahati nasibu inayolitikisa kabumbu na ambayo kipeo chake hakuna anaewwza kuagulia.Gazeti la Die Welt la mjini Berlin linaandika:


Kwenye mabunda ya mali,rushwa haiko mbali.Hata hivyo nchini Ujerumani hakuna bado sheria ya kupambana dhidi ya udanganyifu katika michezo .Ndio maana matapeli tangu wa ndani mpaka wa nje wanaitumia hali hiyo kwasababu wanatambua hatua za kupambana na visa kama hivyo vya udanganyifu ni dhaifu.

Gazeti la West Deutsche Allgemeine linaandika:

Kabumbu ndilo linaloangukia mhanga wa visa kama hivyo.Matapeli wamelitumia kabumbu kujitajirisha.Ni wahalifu wanaobidi kuandamwa kisheria.Na hilo ndilo linalotokea.La muhimu ni kufichua ukweli ,na wahalifu kuwahukumu,tena wote.

Gazeti la "Finacial Times Deutschland linaandika:

"Maafisa wa dimba wanastahiki pia kulaumiwa:Wanafikiri hatua zinazochukuliwa ndizo zitakazomaliza mgogoro wa matapeli katika spoti.Wanajidanganya wenyewe au wanafanya uzembe.Kwasababu hata katika kesi ya Hoyzer ilijulikana wazi kabisa kwamba tatizo hili haliwezi kufumbuliwa katika daraja ya kitaifa wala Ulaya.Watu wanatumia mtandao wa internet kuashiria pambano litakua vipi barani Asia,Uturuki au Ujerumani.Tunaweza kukataza na kupiga marufuku tutakavyo humu nchini.Lakini ni ndoto kuamini matapeli wanaweza kufyekwa moja kwa moja katika fani ya michezo,seuze katika mchezo wa wenye kulipwa ambako suala sio tuu nani atashinda na nani atashindwa-bali zaidi kuliko yote nani atatajirika.Hata hivyo pande zote zinabidi zishirikiane kuhakikisha visa vya udanganyifu angalao vinapungua.

Deutsche Bahn hat einen Vertrag für ein Milliardenprojekt im Wüstenstaat Katar unterschrieben
Kutoka kushoto,mkuu wa shirika la usafiri wa reli la Ujerumani Rüdiger Grube,waziri wa usafiri Peter Ramsauer na waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Qatar Khalid Bin Mohamed Al-AttiyahPicha: dpa

Mada yetu ya pili inahusu kandarasi yenye thamani ya mabilioni ya yuro kwaajili ya ujenzi wa njia ya reli katika nchi tajiri kwa mafuta-Qatar katika Ghuba.Gazeti la RECKLINGHÄUSER Zeitung linaandika:

Mkataba huo uliotiwa saini Doha utasaidia kuinua biashara ya nje ya Ujerumani na wakati huo huo kubuni nafasi zaidi za kazi humu nchini.Majirani wa Qatar ambao pia wanaonyesha kuvutiwa na teknolojia hiyo ya Ujerumani wataangalia vilivyo kuona jinsi wajerumani wanavyofanya kazi yao na kama usemi "Made in Germany" bado ni sahihi.Ikiwa Deutsche Bahn watapasi mtihani huo basi kandarasi zaidi zitawasubiri kutia saini.

Mada yetu ya mwisho inaturejesha katika jimbo hili la North Rhine westphalia ambako uchaguzi wa jimbo unatazamiwa msimu wa mapambazuko mwakani.Gazeti la mjini Cologne,"Express" linaandika:

Ingawa imesalia takriban miezi sita hadi uchaguzi wa bunge katika jimbo la NRW,hata hivyo makadirio ya maoni ya umma kwa serikali inayotawala ya muungano wa nyeusi na manjano,inayoongozwa na waziri mkuu Rüttgers si ya kuvutia.Kwa mujibu wa maoni ya umma vyama vinavyounda serikali hiyo vya CDU na FDP vitapungukiwa na asili mia nane nukta nane ya kura.Lakini hata SPD wataondoka patupu wakipoteza asili mia saba.Kasheshe ile ile iliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa september 27 iliyopita.Vyama vya umma vinapoteza kura na vinavyofaidikia ni vyama vidogo.Vyama vya umma kwa hivyo vinalazimika kujirekebisha ili kuipindua sura hiyo ya mambo.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir (Inlandspresse)

Mhariri:Abdul-Rahman