Kabul.Wanajeshi wawili wa NATO wauwawa huko Afghanistan.
31 Oktoba 2006Matangazo
Wanajeshi wawili wa jeshi la kulinda amani la NATO wameuwawa katika jimbo la Nuristan mashariki mwa Afghanistan.
Afisa wa jeshi la kulinda amani nchini Afghanistan ISAF amesema, wanajeshi hao wameuwawa wakati gari waliyokuwa wakisafiria ilipokanyaga bomu la kutegwa pembezoni mwa bara bara.
Hadi hivi sasa haijafahamika wanajeshi hao ni raia wa nhi gani, lakini vikosi vya kijeshi vya Marekani ndivyo vinavyoshikilia sehemu kubwa ya jeshi la NATO katika nchi hiyo.