KABUL.Wanajeshi wanne wa NATO wauwawa
18 Septemba 2006Matangazo
Mlipuaji wa kujitoa muhanga nchini Afghanistan amewauwa wanajeshi wanne wa NATO na watu wengine kadhaa.
Shambulio hilo limetokea kusini mwa jimbo la Kandahar ambako wanajeshi wa Kanada walikuwa katika zoezi la kugawa kalamu na madaftari kwa watoto.
Maafisa wa Nato wamefahamisha kuwa mtu huyo aliiendesha pikipiki yake katikati ya wanajeshi wa NATO na kisha kujilipua.
Shambulio hilo limetokea siku mbili tu tangu makamanda wa NATO walipotangaza kuwa wamekamilisha zoezi la wiki mbili dhidi ya wapiganaji wa Taliban huko kusini mwa Afghanistan.