KABUL:wanajeshi wa kikosi cha NATO wauwawa
28 Juni 2007Matangazo
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameushambulia msafara wa kikosi cha wanajeshi wa NATO katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan.
Wanajeshi wawili wameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa.
Shambulio jingine kama hilo limewajeruhi raia wawili mashariki mwa mji wa Kabul kwa mujibu wa taarifa za polisi.
Kikosi cha NATO kimethibitisha kwamba askari waliouwawa ni raia wa Marekani na Nepal.