Kabul:Msafara wa NATO washambuliwa.
4 Agosti 2006Matangazo
Msafara wa ulinzi wa NATO umeripuliwa na mtu wa kujitoa muhanga kwa gari huko nchini Afghanistan katika kijiji cha kusini cha kitongoji cha Kandahar.
Hakuna taarifa sahihi ikiwa kuna mwanajeshi yeyote aliyefariki, maana jeshi la NATO halijasema lolote kuhusiana na tukio hilo.
Bomu hilo limetokea siku moja baada ya shambulio la ghafla katika kitongoji hicho kuuwa raia 21 na wanajeshi wanne wa kigeni.
Wataliban wamepanua mashambulizi yao upande wa kusini baada ya majeshi ya NATO kuchukua nafasi ya majeshi ya Marekani siku ya Jumatatu katika operesheni yake kubwa ya ardhini katika historia.
Afghanistan hivi sasa imekuwa katika mashambulizi ya mabomu ya mara kwa mara tangu pale Marekani ilipouondosha utawala wa Taliban mnamo mwaka 2001.