KABUL:Kiongozi mmoja wa al Qaeda atoroka jela ya kijeshi ya Marekani.
3 Novemba 2005Matangazo
Maofisa wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wametangaza kuwa kiongozi mmoja mwandamizi wa kikundi cha al- Qaeda,alitoroka katika jela ya kijeshi ya Marekani nchini Afghanistan majira ya kiangazi yaliyopita na hadi sasa bado anatafutwa.
Mtu huyo raia wa Kuwait ambaye alikamatwa nchini Indonesia mwaka 2002 na kukabidhiwa kwa Marekani,alikuwa ni mmoja wa wafungwa wanne waliofanikiwa kutoroka jela yenye ulinzi mkali katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Bagram mwezi wa Julai
Jela hiyo ya Bagram imewahifadhi mamia ya watuhumiwa,tangu majeshi ya Marekani na marafiki zake,walipoifurusha madarakani serikali ya Taliban nchini Afghanistan mwaka 2001.