Kabul.Jeshi la NATO lawauwa watu 55 wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo.
31 Oktoba 2006Matangazo
Jeshi la kulinda amani la NATO limesema kuwa, vikosi vyake huko kusini mwa Afghanistan yamewauwa watu 55 wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo katika mashambulizi ya saa sita katika jimbo la Zabul.
Aidha mwanajeshi mmoja wa jeshi la kulinda amani nchini Afghanistan ISAF ameuwawa katika mashambulizi hayo.
Shambulio hili limefanywa baada ya lililofanywa mapema siku ya Jumapili ambalo lilipelekea kuuwawa kwa watu 70 wanaoshukiwa kuwa ni wanamgambo baada ya ISAF kukishambulia kituo cha wanamgambo.