Kabul. Wawili wauwawa kwa bomu NATO.
13 Aprili 2007Matangazo
Wanajeshi wawili wa jeshi la NATO wameuwawa kwa bomu lililotegwa kando ya barabara mashariki ya Afghanistan.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la ISAF nchini Afghanistan haikutoa utaifa wa wanajeshi hao.
Maafisa wa jeshi la Marekani , wakati huo huo wamesema kuwa kiasi cha waasi 24 wa Taliban wameuwawa katika shambulio la anga kusini mwa nchi hiyo.