KABUL: Wataliban 200 wameuawa na majeshi ya NATO
4 Septemba 2006Matangazo
Zaidi ya wapiganaji 200 wa Taliban wameuawa katika mashambulio makubwa yaliyotokea katika wilaya ya kusini ya Kandahar.Taarifa hiyo imetolewa na NATO na ikaongezea kuwa wanajeshi 4 wa Kanada pia waliuawa katika mapigano hayo,ambayo ni makubwa kabisa kupata kutokea tangu NATO kupokea dhamana ya kulinda eneo la kusini tangu tarehe 31 mwezi wa Julai kutoka majeshi ya madola shirika yaliyokuwa yakiongozwa na Marekani.Siku ya Jumamosi,shirika la NATO lilipoteza wanajeshi 14 wa Kingereza katika ndege ya upelelezi iliyopata ajali.Maafisa wamesema tatizo la kiufundi ndio limesababisha ajali ya ndege hiyo na haikuangushwa kama ilivyodaiwa na Wataliban.